Wapi Unapata Asali nzuri Zaidi Tanzania , Wauzaji Wa Asali Washauriwa Kuhakikisha Usalama kwa Walaji

News

Tanzania ni Miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa asali Duniani, ata hivyo asali ya Tanzania
imeendelea kufanya vizuri katika masoko mbalimbali ya ndani na nje ya Mipaka ya Tanzania.
JAMBO ASALI ni asali bora ambayo imeendelea kufanya vizuri kwenye masoko ya ndani na
Nje ya Tanzania, Pamoja na kufanya vizuri, wauzaji na wazalishaji wa asali Tanzania
wanapaswa kuzingatia usalama wa asali zao kwa walaji.

Asali nzuri zaidi Tanzania kutoka Jambo Asali

Mlaji au mtumiaji wa asali anatakiwa kuwa na uhakika na usalama wa asali anayo tumia .
Jambo asali ni moja ya kampuni ambayo imekuwa msitari wa mbele kuhakikisha mlaji au
mtumiaji wa asali anakuwa na uhakika wa asali hiyo pindi anapo inunua. Kupitia mfumo
maalumu wa ufuatiliaji, mlaji wa asali anaweza kufuatilia mnyororo mzima wa asali hadi
inapomfikia mezani kwake. Ata hivyo mamlaka balimbali nchini zinaendelea kusimamia ubora
na usalama wa asali kwa mlaji ili kuweza kukuza zaidi biashara za asali bila kuathiri afya za
wateja.
Kama wafanyabiashara wa asali Tanzania tunatakiwa kuwa msitari wa mbele kuhakikisha
usalama wa asali tunayo uza kwa wateja wetu imezingatia afya ya mlaji. Usalama wa asali
unaanzia kwenye uandaaji wa mashamba maalumu ya kufugia nyuki hadi hatua ya mwisho ya
usafirishaji.


Musiba Paul Kitema
Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Jambo Asali Tanzania

Share This :