Usafirishaji wa Asali Nje ya Nchi kutoka Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye sifa kubwa duniani kwa uzalishaji wa asali ya asili yenye ubora wa hali ya juu. Eneo la ikolojia la Miombo Woodlands, milima yenye misitu minene, na mashamba yenye mimea yenye maua mbalimbali, yote huchangia kutoa malisho bora kwa nyuki na hatimaye kuzalisha asali yenye ladha na harufu ya kipekee. Kwa miaka ya hivi karibuni, sekta ya ufugaji nyuki nchini imepiga hatua kubwa, si tu katika kuzalisha kwa wingi, bali pia katika kuuza bidhaa hizo kwenye masoko ya kimataifa. Usafirishaji wa Asali Nje ya Nchi unagusia moja kwa moja chapa ya JAMBO ASALI ambayo imekuwa msitari wa mbele katika kuhakikisha asali ya Tanzania inasafirishwa nje ya nchi hadi Mataifa ya Ulaya.

Miongoni mwa majina yanayong’ara katika biashara hii ni JAMBO ASALI, chapa ya kampuni ya Tanzania International Bee Co. Ltd. Kampuni hii imejitengenezea nafasi kubwa katika ramani ya dunia kwa kusafirisha asali yenye viwango vya kimataifa kwenda Ulaya, Asia, na Mashariki ya Kati (Dubai).
Safari ya JAMBO ASALI Kutoka Shambani Hadi Nje ya Nchi
JAMBO ASALI huzalishwa kupitia mtandao wa wafugaji nyuki wadogo na wakubwa wanaoshirikiana na kampuni, hasa katika mikoa maarufu kwa uzalishaji wa asali kama Tabora, Singida, Kigoma, na Katavi. Baada ya kuvunwa, asali huchakatwa kwa teknolojia za kisasa katika kwenye viwanda vya Sikonge-Tabora na Kibondo-Kigoma na viwanda rafiki vilivyosajiliwa na kuthibitishwa na mamlaka husika kama TBS (Shirika la Viwango Tanzania) na TFDA.
Baada ya kuchakatwa na kupimwa ubora, asali huwekwa kwenye vifungashio vya viwango vya kimataifa, kisha husafirishwa kwa meli au ndege kuelekea masoko ya kimataifa. JAMBO ASALI imefanikiwa kusambaza maelfu ya kilo za asali kwenye masoko haya, ikiwemo:
- Ulaya: Italia, Ujerumani, Lithuania, Kosovo, ireland,Finland, Netherlands na Ufaransa
- Asia: China, Japan, na Korea Kusini
- Mashariki ya Kati (Dubai): Soko la kifahari linalothamini bidhaa za asili zenye ubora kama Jambo asali
Sababu za Mafanikio ya JAMBO ASALI Kwenye Masoko ya Kimataifa
- Ubora wa asali wa Hali ya Juu (High qaulity of Jambo asali)
JAMBO ASALI inajulikana kwa ladha yake ya kipekee, rangi ya dhahabu, na harufu safi inayotokana na mimea ya asili. Asali hii haina kemikali wala vihifadhi, jambo linaloifanya kuvutia wateja wanaopendelea bidhaa za asili. - Uthibitisho wa Viwango (Quality control)
Kampuni inafuata masharti yote ya usafirishaji, ikiwa ni pamoja na quality certification, organic certification, na vipimo vya viwango vya unyevunyevu, sukari, na uchafu. - Ushirikiano na Wafugaji Nyuki wa Kijijini (Community engagement)
JAMBO ASALI hufanya kazi na mamia ya wafugaji nyuki wadogo, ikiwapatia mafunzo, vifaa, na masoko ya uhakika. Hii si tu inaongeza uzalishaji, bali pia huleta manufaa ya moja kwa moja kwa jamii za vijijini. - Mbinu Endelevu za Uzalishaji (Sustainable beekeeping practices)
Ufugaji nyuki hufanyika bila kuharibu mazingira, huku kampuni ikihamasisha upandaji wa miti na kulinda maeneo ya malisho ya nyuki.
Umuhimu wa Usafirishaji wa Asali kwa Uchumi wa Tanzania
Usafirishaji wa asali nje ya nchi una mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa taifa. Sekta hii inasaidia kuongeza mapato ya fedha za kigeni, kutoa ajira, na kupanua wigo wa bidhaa za Tanzania kwenye soko la dunia. JAMBO ASALI ni mfano wa jinsi ubunifu, uaminifu, na ubora unavyoweza kupeleka bidhaa za kijijini hadi kwenye meza za kifahari Ulaya, Asia, na Dubai.
Kampuni pia inachangia kwenye harakati za kutangaza jina la Tanzania kama hub ya bidhaa za nyuki, jambo linaloongeza nafasi ya sekta hii kukua na kuvutia uwekezaji zaidi.
Changamoto na Fursa
Ingawa sekta ya usafirishaji wa asali inakua kwa kasi, bado kuna changamoto kama:
- Gharama kubwa za usafirishaji wa kimataifa
- Mabadiliko ya kanuni za uingizaji wa bidhaa kwenye nchi lengwa
- Uhitaji wa branding na uuzaji wenye nguvu zaidi
Hata hivyo, fursa zilizopo ni nyingi. Soko la dunia lina kiu ya bidhaa asilia, zenye ubora wa juu, na zinazozingatia afya vigezo ambavyo JAMBO ASALI tayari inakidhi.
Hitimisho
Usafirishaji wa asali kutoka Tanzania kwenda masoko ya kimataifa ni ishara ya ukuaji wa sekta ya ufugaji nyuki na ubunifu wa wajasiriamali wa Kitanzania. JAMBO ASALI, kupitia Tanzania International Bee Co. Ltd, imeonyesha njia kwa kuthibitisha kuwa asali ya kijijini inaweza kufika na kushindana kwenye soko la dunia.
Kwa kuendeleza ubora, ushirikiano na wafugaji nyuki, na kuwekeza kwenye teknolojia, Tanzania inaweza kuwa miongoni mwa viongozi wa dunia katika biashara ya bidhaa za nyuki. JAMBO ASALI imejipanga kuendelea kusambaza ladha halisi ya Tanzania kutoka mzinga hadi ulimwengu.

