JAMBO ASALI ni asali inayo zalishwa Tanzania kutoka kwenye misitu ya asili inayo
hifadhiwa na kwa kulinda na kuhifadhi mazingiraya asili. JAMBO ASALI ni asali inyo ongoza
kwa ubora yenye kiwango kikubwa cha ubora na usalama kwa mlaji, Jambo asali inapitia
mifumo yote ya kiusalama na kuzingatia uhifadhi wa mazingira.
Wazalishaji wa jambo asali wamepitia mafunzo ya kitaalamu ya kuandaa mizinga iliyo bora,
kuandaa mashamba maalumu yaliyo tengwa kwa ajili ya ufugaji wa nyuki, wamepitia mafunzo
ya namna bora ya kusimamia na kuratibu mnyororo mzima wa asali hadi inapofikia kiwandani
kwa ajili ya uchakataji wa mwisho. Ata hivyo asali ya jambo inapofika kiwandani, wataalamu
waliopitia mafunzo wanasimamia kanuni za ubora katika uchakataji na ufungashaji wa asali
kabla ya kuisafirisha Kwenda kwa walaji.
Kutokana na mnyororo huu, JAMBO ASALI imekuwa asali namba moja kwa ubora wa hali
ya juu kuliko asali zote Tanzania. Hii imesababisha JAMBO ASALI kupendwa na walaji wengi
kwa kutumiwa katika matumizi ya kila siku ikiwa ni Pamoja na kutumiwa kama mbadala wa
Sukari ya kiwandani.
JAMBO ASALI imeendelea kutumika pia katika matumizi ya kiafya katika mwili wa
mwandamu, watu mbalimbali wanatumia JAMBO ASALI katika matibabu ya vidonda sugu,
matibabu ya vidonda vya tumbo, na matumizi mbalimbali, ata hivyo wataalamu wa afya pia
wameanza kushauri watu mbalimbali kuwa na utamaduni wa kutumia asali katika Maisha ya
kila siku kwakuwa asali ina faida nyingi sana katika mwili wa Mwanadamu.
FROM TANZANIA’S FORESTS TO EUROPEAN TABLES
